Friday, October 17, 2008

WIMBO WA TAIFA

Ama kweli yale mawazo ya kusema eti hip hop ni uhuni yamepitwa na wakati kwani hivi sasa tunashuhudia muziki huo unaelezea matatizo yanayoikumba jamii kwa kiasi kikubwa tofauti na watu walivyo fikiria.Juzi juzi tu msanii wa hip hop Kala Jeremiah akishirikana na mwana dada Nakaaya Sumari aliutambulisha wimbo wake unaoitwa "Wimbo wa taifa",wimbo ambao kwa kiasi kikubwa unaelzea mztatizo yaliyopo nchini,matatizo ambayu kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na Serikali yetu.Katika wimbo huo,Kala amejaribu kuonyesha hisia zake kwa Serikali na kuhoji je,Nyerere angekuepo mungefanyaje?na je,angefurahia hali iliyopo nchini?Mimi binafsi nawapongeza sana Kala na Nakaaya kwa kuonyesha mfano mzuri na wa kuigwa na wasanii wengine,kwani msanii ni kioo cha jamii hivyo anatakiwa kutunga nyimbo za kuelimisha jamii na si kila leo kuona wasanii wetu wakiimba starehe,kujirusha,wanawake na mambo mengine yasiyo na msingi wowote na yanayopelekea muzik huo kuonekana wa kihuni.

No comments:

vipi umeipenda blog yangu?