Monday, October 13, 2008

HUU NI UTAMADUNI AU???


Kuna kitu kinaniumiza sana,kitu hicho sikingine bali ni kigeugeu chetu sisi Watanzania.Sisi Watanzania tunajifanya ni watu tunaotetea na kukuza mila na desturi zetu kwa kuhakikisha hilo asasi na taasisi mbali mbali zinazohusika na maswala ya utamaduni,mila na desturi zimekuwa mstari wa mbele katika kuhakiisha tunatunza na kuzifuata desturi na mila zetu.Moja kati ya harakati za taasisi hizo katika kulinda na kutetea mila na desturi zetu ni kukemea uvaaji mbaya ambao tunaamini siyo desturi yetu Watanzania kuvaa hivyo.Matharani,kuna haka katabia cha madada zetu kuvaa vivazi vya nusu uchi,tabia hii na nyingi nyenginezo ninapingwa vikali na taasisi hizo katika kuhakikisha mambo yanaenda sawa.Mimi napenda kugusia hili swala la mavazi,kwanza hebu tuziangalie picha za hapo juu,Kwa haraka haraka tu utaona ni afadhali mavazi ya kina dada wa picha ya kwanza ingawa hayana afadhali kitu.Cha kushangaza taasisi hizo zinakemea madada kuvaa vivazi vya ajabu mitaani lakini wakati huo huo wanahusika kuunga mkono mashindano mbalimbali ya ulimbwende!sisemi kwamba wanakosea,hapana kwani ulimbwende ni moja ya sanaa ila katika mashindano hayo hayo kuna mavazi yanayo valiwa si ya kistaarabu.Mfano kwenye picha za hapo juu,picha ya pili inamuonesha miss Tanzania mwaka 2008 bibie Amanda Ole Sulul na picha ya tatu inamuonesha bibie Flaviana Matata (miss universe 2008) wote wakiwa na vivazi vya ufukweni.Swali linakuja je,mavazi yao yanaendana na mila na desturi za Mtanzania?Nataraji jibu litakuwa hapana,Sasa je hizo taasisi zimefanya uamuzi wa busara kuunga mkono ama kuyatambua mashindano ya urembo?
hayo ni maswali machache ambayo Watanzania inatubidi tujiulize kuhusiana na hili swala la ulimbwende.

No comments:

vipi umeipenda blog yangu?