Monday, October 13, 2008

MTANZANIA

Kusema ukweli hali ya maisha ni ngumu.Na ugumu huu wa maisha unatokana na utawala mbovu na ubinafsi uliokithiri ndani ya Serikali hasa hii ya wamu ya nne(4),kwa mfano ndani ya mwaka huu mmoja wa 2008 tumeona matukio mengi ambayo yameikumba napengine kuitikisa serikali.Miongoni mwa matukio hayo ni kuhsu sakata la Richmond na lile la ufisadi uliofanywa na akaunti ya kulipa madeni ya nje yaani EPA,matukio haya yamechangia ama kusababisha kujiuzuru kwa aliyekuwa waziri mkuu Mh. Edward Lowasa na mawaziri wengine wawili.Lakini nia yangu hasa ni kuelezea nini ama nani chanzo cha yote haya,mi kwa mawazo yangu naona hakuna haja ya kumtafuta mchawi wakati tunaye sisi wenyewe.Lawama zangu kwa kiasi kikubwa nazielekeza kwa wananchi sisi wenyewe kwa kutokubali mabadiliko,ndio!Namaanisha kuwa kuna ulazima wa kufanya mabadiliko ya serukali kwa maana hii serikali iliyopo madalakani imeshindwa kufanya mabadiliko,kwani badala ya kuangalia uchumi wa Tanzania unaendaje wao wapowapo tu na wanaendelea kuzitafuna fedha za umma bila ya aibu!Jambo lingine linaloniumiza kichwa ni kwamba,je hizi fedha wanazotumia CCM kununua khanga,t-shirt na kapelo zingetumika kuwapa mikopo wakina mama na vijana wasio na ajira si angalau tungelisukuma mbele gurudumu letu la maendeleo .Siyo siri Watanzaia wenzangu kuna haja ya kujipanga upya ili tusije rudia makosa tuliyofanya ama sivyo tutabaki TUKILIA NA KUSAGA MENO!!

No comments:

vipi umeipenda blog yangu?