Monday, October 20, 2008
HEBU CHUKUA HIYO!!
Katika pita pita zangu kwenye mtandao fulani hivi nikakutana na hii katuni ya bwana Nathan Mpangala,katuni inaonesha Chama Cha Mapinduzi(CCM) kikihangaika kumteketeza mdudu rushwa kwenye uchaguzi wakati mdudu huyo yupo nyuma yake.Je,watafanikiwa?Ukweli hawawezi hadi wawamalize mafisadi wote ndani ya chama chao halafu ndio wawaangalie wale wa nje,Hata kwa wale waumini wa dini ya kikristo wataungana na mimi pale Yesu aliposema "ni unafiki kuhangaikia kibanzi kwenye jicho la mwenzako ilhali we mwenyewe una bolti jichoni".Ni heir CCM wawashughulikie mafisadi walio ndani ya chama kwanza kisha wengine watafuata .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment