Kitendo cha msanii wa Bongo fleva Haroun Kahena almaarufu Inspecta Haroun "babu" kujibu wimbo mwingine wa msanii maarufu wa hip hop nchini Mwana FA a.k.a Binamu unaoitwa "bado nipo nipo kwanza" kimewakasilisha wadau na mashabiki wengi wa muziki huo na kudai kuwa mkongwe huyo ameishiwa.
Kauli hiyo ya mashabiki ya kumzodoa mkongwe huyo inatokana na Inspecta kuonekana kuzoea tabia ya kujibu mashairi ya nyimbo za watu na kufananishwa na waimbaji wa taarabu!wakiongea na chanzo chetu cha habari mashabiki hao walisema "Kama kashindwa kuimba bongo fleva bora arudi bush akalime mihogo!" na kuongezea kuwa "Sisi kama washabiki tumemchoka kwa sababu Mwaka wa shetani kajibu,huu nao wa Mwana FA kajibu imekuwa kama taa rabu sasa".Haya Inspecta KALAGHABAHO!Habari ndo hiyo,kaza buti urudi kwenye chati ama sivyo utaambulia patupu!!!
Friday, October 17, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment