Wednesday, November 5, 2008
ERNESTO "CHE" GUEVARA
Ernesto "che" Guevara ni mmoja wa waasisi wa taifa la Cuba aliye uawa katika mapambano kati ya vikosi vya msituni vya Cuba vikipambana.Che guevara ni mmoja ya watu ambao ni kielelezo cha amani duniani kwani yeye mwenyewe alikuwa na imani kali za kirastafari.Rest in peace.
VIVA MANDELA
Nelson Mandela ni rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini,rais huyu ana historia ya pekee kwani amekaa jela miaka 21!hii yote ni kwa sababu ya juhudi zake za kutafuta uhuru wa nchi hiyo.Kingine kinachosikitisha zaidi ni kwamba,Marekani iliwahi kumtaja Mandela kama mmoja kati ya magaidi wa ulimwengu! eti kwa sababu aliwahimiza wafuasi wa chama chake kuandamana na kugoma ili kudai uhuru wao.Lakini cha kufurahisha ni kwamba Dunia nzima sasa inamtumia Mandela kama kielelezo cha uhuru na kupinga ubaguzi.
SONGEA TEACHERS TRAINING COLLEGE
HONGERA BARACK OBAMA
Leo ni siku ya kihistoria kwa Taifa kubwa Duniani la Marekani kwani kwa mara ya kwanza taifa hilo linaongozwa na rais kijana zaidi mwenye umri wa miaka 43,lakini cha kufurahisha zaidi ni kwamba,kwa mara ya kwanza kwa taifa hilo kuongozwa na rais mweusi ama mwenye asili ya Afrika!!
Kwa kweli ni furaha ilioje,Mr. Obama alikuwa akiubiri mabadiliko kwenye kampeni zake,sasa tukae tusubiri mabadiliko.
Kwa kweli ni furaha ilioje,Mr. Obama alikuwa akiubiri mabadiliko kwenye kampeni zake,sasa tukae tusubiri mabadiliko.
Tuesday, October 21, 2008
Monday, October 20, 2008
KING OF HIP HOP
Kwa hakika mimi kama mdau wa muziki wa hip hop nchini utakapo niuliza ni nani anafaa kuwa mfalme wa Hip hop Afrika mashariki na kati,nitakujibu Farid Kubanda a.k.a Fid Q.Siyo siri jamaa amesimama pande zote,namaanisha uandiahi wa mistari,kupangilia vina na hata ku-flow na beat!vitu hivi na vingine vingi ndio vinanifanya nimkubali jamaa kama mfalme wa kweli wa hip hop nchini.I MEAN FID Q hupo juu kama povu la bia!!!
HEBU CHUKUA HIYO!!
Katika pita pita zangu kwenye mtandao fulani hivi nikakutana na hii katuni ya bwana Nathan Mpangala,katuni inaonesha Chama Cha Mapinduzi(CCM) kikihangaika kumteketeza mdudu rushwa kwenye uchaguzi wakati mdudu huyo yupo nyuma yake.Je,watafanikiwa?Ukweli hawawezi hadi wawamalize mafisadi wote ndani ya chama chao halafu ndio wawaangalie wale wa nje,Hata kwa wale waumini wa dini ya kikristo wataungana na mimi pale Yesu aliposema "ni unafiki kuhangaikia kibanzi kwenye jicho la mwenzako ilhali we mwenyewe una bolti jichoni".Ni heir CCM wawashughulikie mafisadi walio ndani ya chama kwanza kisha wengine watafuata .
BIG UP A.Y
HIP HOP 4 HEALTH
Saturday, October 18, 2008
HISTORIA FUPI YA BOB MARLEY
Alikataa kuandika urithi kwa kuamini kuwa marastafari huwa hawafi
Robert Nesta Marley,ambaye baadaye alikuja kujulikana kama Bob Marley,alizaliwa Februari 6,1945 katika kijiji cha Nine Mile kwenye Parishi ys mtakatifu Ann huko Jamaica.Baba yake Norval Sinclair Marley alikuwa mzungu na mama yake Cedelia Booker alikuwa Mjamaica mweusi.
Historia ya maisha yake haitofautiani sana na wanamuziki wenzake wa reggae Peter Tosh aliyelelewa na shangazi yake na Bunny Wailer aliyelelewa na baba yake zaidi,ni historia ya huzuni iliyo muacha Bob Marley chini ya mzazi mmoja(mama yake) pale alipofiwa na baba yake akiwa na umri wa miaka kumi tu.Norval Sinclair (baba yake Bob Marley) alikuwa nahodha wa meli na muangalizi wa mashamba,alikufa mwak 1955 akiwa safarini,wakati huo alikuwa na umri wa miaka 60.
Kifo hicho kilimfanya mama yake Bob Markey ahamishe makazi kwenye mji wa Kingston,huko Bob alikutana na Bunny Wailer wakawa marafiki na kujifunza muziki pamoja.Akiwa na umri wa miaka 14,Bob Marley aliacha shule na kujiunga na chuo cha ufundi wa kuchomelea vyuma,muda wakewa kupumzika alikuwa na Bunny Wailer kwenye muziki,kipindi hiko mwalimu wao alikuwa Joe Higgs,muimbaji wa mtaani mwenye imani ya kirastafari.Chini ya Joe Higgs walikutana na Peter Tosh na kuungana naye.
Mwaka 1962 Bob Marley alirekodinyimbo zake mbili za kwanza ambazo ni;"Usihukumu"(judge not) na "kikombe kimoja cha chai"(one cup of tea) chini ya muandaaji Leslie Kong,lakini nyimbo hizo hazikukubalika sana.Mwaka 1963 akashirikiana na Bunny Wailer,Peter Macintosh(Peter Tosh),Junior Braithwaite,Beverly Kelso na cherry Smith n kuunda kundi la "The Teenagers" kundi hilo lilijibadili majina na kuwa "The wailing rude boys","The wailling wailers" na mwishowe "The wailers".Mwaka 1964 na 1965 watoa vibao vikali kama "Usiwe na wasiwasi"(simmer down) na "Nafsi isiyokubali"(soul rebel)nyimbo hizi zilikonga nyoyo za Wajamaika wengi.Hata hivyo kufikia mwaka 1965 lilibakiwa na wakali watatu tu,yaani Bob Marley,Bunny Wailer n Peter Tosh,baada ya wengine kujiengua.Mwaka 1966 Bob Marley alimuoa kimwana Rita Anderson na kwenda kuishi kwa muda na mama yake huko Wilmington,Delaware nchini Marekanina kuibuka na imani kali ya kirastafari na kuja na mtindo wa kufuga nywele uitwao "dreadlocks".Baada ya hapo Bob Marley na kundi lake la The wailers walitoa vibao kemkem vilivyoitikisa Dunia.Kati ya vibao hivyo ni;Africa unit,Zimbabwe,Could oyu loved?,Iron lion zion,Is this love,Buffalo soldier na vingine vingi.Huyo ni Bob Marley,mfalme wa reggae aliyepinga ubaguzi kwani hata yeye mwenyewe alisema "Wananiita chotara,lakini mimi siegamii upande wowote bali nipo upande wa Mungu aliye niumba kutoka kwa weusi na weupe".Hiyo ni biograph ya mwanaharakati huyo wakupinga ubaguzi."REST IN PEACE RASTAFARAE"

Friday, October 17, 2008
HAWA NDIO WENYE UTAMADUNI ULIO HAI
Kusema kweli Masaai ni moja ya makabila machache yaliyobakia na utamaduni ulio hai barani Afrika,Wamasai wenyewe wamukuwa kipaumbele katika kulinda na kuutetea utamaduni wao,mfano hadi muda huu wamasai wanaendelea kuenzi shughuli mbalimbali zinazosaidia katika kulinda utamaduni wao,baadhi wa shughuli hizo ni kama sherehe za kimila,jando na shughuli nyingine mbalimbali za kimila.
WIMBO WA TAIFA
Ama kweli yale mawazo ya kusema eti hip hop ni uhuni yamepitwa na wakati kwani hivi sasa tunashuhudia muziki huo unaelezea matatizo yanayoikumba jamii kwa kiasi kikubwa tofauti na watu walivyo fikiria.Juzi juzi tu msanii wa hip hop Kala Jeremiah akishirikana na mwana dada Nakaaya Sumari aliutambulisha wimbo wake unaoitwa "Wimbo wa taifa",wimbo ambao kwa kiasi kikubwa unaelzea mztatizo yaliyopo nchini,matatizo ambayu kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na Serikali yetu.Katika wimbo huo,Kala amejaribu kuonyesha hisia zake kwa Serikali na kuhoji je,Nyerere angekuepo mungefanyaje?na je,angefurahia hali iliyopo nchini?Mimi binafsi nawapongeza sana Kala na Nakaaya kwa kuonyesha mfano mzuri na wa kuigwa na wasanii wengine,kwani msanii ni kioo cha jamii hivyo anatakiwa kutunga nyimbo za kuelimisha jamii na si kila leo kuona wasanii wetu wakiimba starehe,kujirusha,wanawake na mambo mengine yasiyo na msingi wowote na yanayopelekea muzik huo kuonekana wa kihuni.
OKOA HIP HOP CAMPAIGN
Usishangae saaana!hao pichani ni baadhi tu ya wasanii wa hip hop nchini Tanzania ambao kwa pamoja wameanzisha kampeni ya kuuokoa muziki wa hip hop,kampeni hiyo iliyo anzishwa na msanii na mtayarishaji wa video,Adili a.k.a Hisabati(wa mwisho chini upande wa kulia) unawajumuisha wasanii wengine wa hiphop kama;Joh Makini,Mansu-ri,Mapacha na Blac.Wengine ni Jay moe,Salu-te,Saigon(mzukaa),Magazijuto,Nako2Nako na Geez Mabovu ambao hawapo pichani.Wasanii hao kwa pamoja wapiga kampeni za kuokoa muziki wa hip hop nchini,muziki ambao unaifunza jamii na kuelezea matatizo mbali mbali yanayo ikumba jamii ya Tanzania.
BIG UP COMEDY ORIGIONAL!!!
Hongera Comedy origional!!Siyo siri nimefurahishwa na kitendo cha iliyokuwa Ze comedy kuachana na mzozo wa muda mrefu kati yao na kituo cha televisheni cha EATV ambacho kilidai kuwa na haki za umiliki wa kikundi hicho.Hatua ya kikundi hicho ambacho hivi sasa kinajiita Comedy origional ya kuanza kurusha vipindi vyake katika kituo cha televisheni cha TBC1kimewafurahisha Watanzania wengi kwani walikuwa wakisubiri kwa hamu show za kikundi hicho.Nawashauri Comedy origional kufanya kazi kwa moyo mmoja ili wawaridhishe Watanzania waliokuwa wanasubria ujio wao.
INSPECTA KAISHIWA!!
Kitendo cha msanii wa Bongo fleva Haroun Kahena almaarufu Inspecta Haroun "babu" kujibu wimbo mwingine wa msanii maarufu wa hip hop nchini Mwana FA a.k.a Binamu unaoitwa "bado nipo nipo kwanza" kimewakasilisha wadau na mashabiki wengi wa muziki huo na kudai kuwa mkongwe huyo ameishiwa.
Kauli hiyo ya mashabiki ya kumzodoa mkongwe huyo inatokana na Inspecta kuonekana kuzoea tabia ya kujibu mashairi ya nyimbo za watu na kufananishwa na waimbaji wa taarabu!wakiongea na chanzo chetu cha habari mashabiki hao walisema "Kama kashindwa kuimba bongo fleva bora arudi bush akalime mihogo!" na kuongezea kuwa "Sisi kama washabiki tumemchoka kwa sababu Mwaka wa shetani kajibu,huu nao wa Mwana FA kajibu imekuwa kama taa rabu sasa".Haya Inspecta KALAGHABAHO!Habari ndo hiyo,kaza buti urudi kwenye chati ama sivyo utaambulia patupu!!!

KIPANYA!!
Ebwana kama kuna mchoraji wa katuni anaye elezea moja kwa moja habari zinazo igusa jamii basi ni Masoud Alli "Kipanya".Huyu jamaa yupo juu sio tu kwenye suala la uchoraji na utangazaji tu!ila huyu jamaa yupo juu hata katika kutafuta "Good life"(kama vijana wanavyoita) kwani juzi juzi tu alizindua mavazi yake ya KP WEAR na Website yake ijulikanayo kama kipanya.co.tz.
Kwa hatua alizofikia bwana kipanya tunaweza kusema kuwa yeye ni mwanamapinduzi halisi wa fani ya uchoraji katuni Tanzania.CONGRATULATION MY BROTHER!!!KEEP IT UP!
Kwa hatua alizofikia bwana kipanya tunaweza kusema kuwa yeye ni mwanamapinduzi halisi wa fani ya uchoraji katuni Tanzania.CONGRATULATION MY BROTHER!!!KEEP IT UP!
Wednesday, October 15, 2008
JE WAJUA?????
Monday, October 13, 2008
HUU NI UTAMADUNI AU???
Kuna kitu kinaniumiza sana,kitu hicho sikingine bali ni kigeugeu chetu sisi Watanzania.Sisi Watanzania tunajifanya ni watu tunaotetea na kukuza mila na desturi zetu kwa kuhakikisha hilo asasi na taasisi mbali mbali zinazohusika na maswala ya utamaduni,mila na desturi zimekuwa mstari wa mbele katika kuhakiisha tunatunza na kuzifuata desturi na mila zetu.Moja kati ya harakati za taasisi hizo katika kulinda na kutetea mila na desturi zetu ni kukemea uvaaji mbaya ambao tunaamini siyo desturi yetu Watanzania kuvaa hivyo.Matharani,kuna haka katabia cha madada zetu kuvaa vivazi vya nusu uchi,tabia hii na nyingi nyenginezo ninapingwa vikali na taasisi hizo katika kuhakikisha mambo yanaenda sawa.Mimi napenda kugusia hili swala la mavazi,kwanza hebu tuziangalie picha za hapo juu,Kwa haraka haraka tu utaona ni afadhali mavazi ya kina dada wa picha ya kwanza ingawa hayana afadhali kitu.Cha kushangaza taasisi hizo zinakemea madada kuvaa vivazi vya ajabu mitaani lakini wakati huo huo wanahusika kuunga mkono mashindano mbalimbali ya ulimbwende!sisemi kwamba wanakosea,hapana kwani ulimbwende ni moja ya sanaa ila katika mashindano hayo hayo kuna mavazi yanayo valiwa si ya kistaarabu.Mfano kwenye picha za hapo juu,picha ya pili inamuonesha miss Tanzania mwaka 2008 bibie Amanda Ole Sulul na picha ya tatu inamuonesha bibie Flaviana Matata (miss universe 2008) wote wakiwa na vivazi vya ufukweni.Swali linakuja je,mavazi yao yanaendana na mila na desturi za Mtanzania?Nataraji jibu litakuwa hapana,Sasa je hizo taasisi zimefanya uamuzi wa busara kuunga mkono ama kuyatambua mashindano ya urembo?
hayo ni maswali machache ambayo Watanzania inatubidi tujiulize kuhusiana na hili swala la ulimbwende.
MTANZANIA
Kusema ukweli hali ya maisha ni ngumu.Na ugumu huu wa maisha unatokana na utawala mbovu na ubinafsi uliokithiri ndani ya Serikali hasa hii ya wamu ya nne(4),kwa mfano ndani ya mwaka huu mmoja wa 2008 tumeona matukio mengi ambayo yameikumba napengine kuitikisa serikali.Miongoni mwa matukio hayo ni kuhsu sakata la Richmond na lile la ufisadi uliofanywa na akaunti ya kulipa madeni ya nje yaani EPA,matukio haya yamechangia ama kusababisha kujiuzuru kwa aliyekuwa waziri mkuu Mh. Edward Lowasa na mawaziri wengine wawili.Lakini nia yangu hasa ni kuelezea nini ama nani chanzo cha yote haya,mi kwa mawazo yangu naona hakuna haja ya kumtafuta mchawi wakati tunaye sisi wenyewe.Lawama zangu kwa kiasi kikubwa nazielekeza kwa wananchi sisi wenyewe kwa kutokubali mabadiliko,ndio!Namaanisha kuwa kuna ulazima wa kufanya mabadiliko ya serukali kwa maana hii serikali iliyopo madalakani imeshindwa kufanya mabadiliko,kwani badala ya kuangalia uchumi wa Tanzania unaendaje wao wapowapo tu na wanaendelea kuzitafuna fedha za umma bila ya aibu!Jambo lingine linaloniumiza kichwa ni kwamba,je hizi fedha wanazotumia CCM kununua khanga,t-shirt na kapelo zingetumika kuwapa mikopo wakina mama na vijana wasio na ajira si angalau tungelisukuma mbele gurudumu letu la maendeleo .Siyo siri Watanzaia wenzangu kuna haja ya kujipanga upya ili tusije rudia makosa tuliyofanya ama sivyo tutabaki TUKILIA NA KUSAGA MENO!!
Subscribe to:
Posts (Atom)